KUTOA PESA kutoka kwenye akaunti au kadi ya prepaid kwa Wakala:

(Ni lazima mteja anayetoa awe ameunganishwa na huduma ya Mobile Banking)

Jinsi ya kutoa pesa kwa wakala kwa njia ya simu:

Iwapo mteja ana simu ya kawaida:

 • Piga *150*34#
 • Ingiza namba yako ya siri ya mobile banking
 • Chagua namba 8 (Toa Pesa)
 • Utapata namba ya kutolea (Token), mpatie wakala ili utoe pesa kutoka kwenye akaunti ama prepaid kadi yako. Namba hii itumike ndani ya dakika 5 tu Muda ukizidi dakika 5, itabidi urudie hatua hizo hapo juu
 • Mtajie wakala namba yako ya simu iliyounganishwa na huduma ya mobile banking
 • Mjulishe wakala kiasi unachohitaji kutoa
 • Wakala atafanya muamala katika machine yake (POS)
 • Muamala ukikamilika, mashine ya wakala itatoa risiti
 • Ujumbe wa uthibitisho wa muamala utatumwa kwenye simu ya mteja
 • Mteja atatakiwa kusaini kwenye daftari la miamala
 • Muamala utakuwa umekamilika

Iwapo Mteja ana BancABC App (Android au ios):

 • Fungua aplikesheni ya BancABC
 • Ingiza namba ya simu iliyosajiliwa kwenye huduma ya mobile banking pamoja na namba ya siri
 • Fungua kitufe cha “Qwikcash (Cardless Withdrawal)”
 • Bonyeza “Tengeneza au Generate” kupata namba ya kutolea (Token)
 • Mpatie wakala ili utoe pesa kutoka kwenye akaunti ama prepaid kadi yako. Namba hii itumike ndani ya dakika 5 tu Muda ukizidi dakika 5, itabidi urudie hatua hizo hapo juu
 • Mtajie wakala namba yako ya simu iliyounganishwa na huduma ya mobile banking
 • Mjulishe wakala kiasi unachohitaji kutoa
 • Wakala atafanya muamala katika machine yake (POS)
 • Muamala ukikamilika, mashine ya wakala itatoa risiti
 • Ujumbe wa uthibitisho wa muamala utatumwa kwenye simu ya mteja
 • Mteja atatakiwa kusaini kwenye daftari la miamala
 • Muamala utakuwa umekamilika

Send Message

Dear Customer, Please let us know your query and we will get back to you as soon as possible.